Kukaribia kwa kilele cha ziara: Atabatu Abbasiyya tukufu yapangilia matembezi ya mazuwaru na kuepusha msongamano

Maoni katika picha
Kutokana na kukaribia kwa kilele cha ziara na kuongezeka watu wanao ingia katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu imeongeza ufanisi katika mkakati wa kuwahudumia mazuwaru, kwa kutumia wafanya kazi wake wote pamoja na wale wa kujitolea, miongoni mwa mikakati iliyo pangwa hapo awali na hivi sasa kwa ajili ya kuondoa msongamano wa mazuwaru ni:

  • - Kugawa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) sehemu mbili, ya wanawake na wanaume.
  • - Kuweka uzio wa mbao wa muda uliogawa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kati ya wanaoingia na kutoka na kufanya uingiaji na utokaji wa mazuwaru kua rahisi.
  • - Dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kutembelewa na wanaume pekeyake, huku sardabu ya Imamu Hussein na Jawaad (a.s) zikitengwa kwa ajili ya wanawake peke yao, sardabu hizo zimewekwa dirisha la kaburi tukufu.
  • - Kuweka idadi kubwa ya waelekezaji ndani na nje ya haram kwa ajili ya kuwaongoza mazuwaru na kuondoa msongamano.
  • - Kuweka vizuwizi vya watu ndani na nje ya haram kwa ajili ya kudhibiti muingiliano wa waingiaji na watokaji.
  • - Kuteua milango maalum ya kuingia na kutoka ndani ya haram tukufu.
  • - Kuweka utaratibu maalum wa kuingia na kutoka mawakibu za waombolezaji bila kusababisha msongamano wa mazuwaru.
  • - Kuongeza idadi ya vizuwizi kwa ukaguzi kwenye milango ya haram tukufu.
  • - Kuongeza sehemu za kuvulia viatu na kutunza viatu bamoja na vifaa vingine (Amanaat).

Kumbuka kua mambo hayo yanaweza kuongezeka baadae kutokana na kuongezeka kwa mazuwaru wanao endelea kumiminika, kadri tunavyo karibia kilele cha ziara, usiku wa mwezi ishirini Safar na mchana wake ndivyo mazuwaru wanavyo endelea kuongezeka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: