Mawakibu za kiarabu na kiajemi zaipongeza Iraq katika kutekeleza ziara ya Arubaini.

Maoni katika picha
Kutokana na ukweli kua Imamu Hussein (a.s) anatukio la kibinaadamu la pekee, linalozidi kilele cha ubinaadamu, makundi ya waumini kutoka kila sehemu ya dunia watu wa mataifa na rangi tofauti, wanakuja kumzuru Imamu Hussein (a.s) na kuhuisha kumbukumbu ya Arubaini, wakishirikiana na raia wa Iraq katika kufanya ziara ya Arubaini.

Ziara ya Arubaini mwaka huu imekua sawa na miaka mingine, upande wa mazuwaru na mawakibu za kuomboleza na kutoa huduma, kuna maukibu nyingi hasa za kuomboleza, ambazo zimeingizwa rasmi katika orodha ya mawakibu na kupewa nafasi rasmi ya kushiriki. Kumbuka kua kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya imetangaza kua mawakibu zilizo shiriki katika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) na kusajiliwa rasmi mwaka huu zimefika (225) maukibu za kutoa huduma na kuomboleza, kutoka nchi (22) za kiarabu na kiajemi, ambazo ni: (Saudia – Kuwait – Baharain – Sirya – Lebanon – Yemen – Oman – India – Iran – Pakistan – Afughanistan – Tailendi – Uturuki – Adharbaijan – Ufaransa – Ujerumani – Swiden – Uingereza – Marekani – Holandi – Kenya – Tanzania)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: