Karbala hivi sasa: Mafuriko ya watu wanaokuja wka vikundi na mmoja mmoja wanaendelea kumiminika bila kuisha.

Maoni katika picha
Baada ya kuanza kuadhimisha ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), mji mtukufu wa Karbala umekua sawa na bahari inayo furika makundi ya binaadamu, wanamiminika katika kaburi lake kupitia vikundi na mtu mmoja mmoja bila kukatika kwa namna isiyo elezeka.

Njia zinazo elekea Karbala bado zimejaa mazuwaru wanao onyesha mapenzi ya hali ya juu kwa Imamu Hussein (a.s) katika kumbukumbu ya Arubaini, historia inashuhudia matembezi yenu na inamtambulisha nani Hussein na wapenzi wake ni wakina nani na ipi Karbala ya Hussein.

Hussein ndio kusudio lao la kwanza na mwisho na kudumisha ziara ya Arubaini ndio kilele chao, kama linavyo ona kila jicho kinacho tokea saa hizi Karbala, mamilioni ya watu wamefurika na kumuomba Mwenyezi Mungu adumishe neema hii.

Atabatu Abbasiyya tukufu inatumia uwezo wake wote kuhakikisha ziara inafanyika kwa amani na utulivu, imeanza mapema na itaendelea leo mchana hadi usiku. Kamera ya Alkafeel imetembelea maeneo mbalimbali ya mazuwaru katika usiku wa Arubaini na inakuletea picha za baadhi ya matukio.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: