Kitengo cha kulinda nidham katika Atabatu Abbasiyya tukufu: Tuliweka mkakati madhubuti uliosaidia kuweka amani katika ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kitengo cha kulinda nidham katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya kazi kubwa ya kuweka amani na utulivu katika ziara ya Arubaini, kitengo kiliweka mkakati maalum wa kuimarisha usalama na kikaanza kuutekeleza tangu siku za kwaza za ziara ya Arubaini.

Tumeongea na rais wa kitengo hicho Ustadh Hussein Ridhwa amesema kua: Kama kawaida msimu wa ziara ya Arubaini unapo karibia, huwa tunafanya mikutano na vyombo vya serikali ya mkoa pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama, huwa tunakua na mawasiliano ya karibu na vyombo vyote vya ulinzi na asalama kabla na wakati wa ziara ya Arubaini, wakiwemo askari wa mkoa wa Karbala waitwao kikosi cha ulinzi wa eneo la katikati ya haram mbili tukufu.

Akaongeza kua: Tumeweka mamia ya watumishi wetu pamoja na watumishi wa kujitolea kutoka nje ya Ataba tukufu wenye uzowefu na kazi hii, wamewekwa kila mahala penye msongamano wa watu ndani na nje ya haram, kwa ajili ya kudhibiti usalama katika maeneo hayo, aidha tunamawasiliano ya karibu na idara ya mawasiliano ya Ataba tukufu, kwa ajili ya kutumia kamera za ulinzi zinazo piga picha matukio yote, watumishi wetu wanawasiliana kwa kutumia redio coll zinazo bebeka kwa urahisi.

Akafafanua kua: Kitengo kimechukua jukumu la kulinda amani katika maeneo yote ya mjini na kwenye barabara zinazo tumiwa na mazuwaru kwa wingi.

Fahamu kua kitengo cha kulinda nidham katika Atabatu Abbasiyya kila ziara kubwa huwa kinachukua jukumu la kulinda amani, na kuhakikisha usalama wa mazuwaru ndani na nje ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: