Rais wa kitengo cha usafirishaji katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Abduljawaad Kaadhim amesema kua wametumia gari (315) zenye ukubwa tofauti, kwa ajili ya kusaidia kubeba watu wanaokuja kuzuru malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi katika kumbukumbu ya Arubaini, kazi hiyo inazaidi ya wiki sasa na kilele chake ni leo (20 Safar) katika barabara muhimu ya (Karbala – Hilla).
Akaongeza kua: “Katika utekelezaji wa ratiba ya usafirishaji tumeshirikiana na muungano wa viwanda vya vyakula pamoja na uongozi wa ndege za kitaifa na magari kutoka kijiji cha Haswiin, tukateua uwanja uliopo karibu na geti la Ibrahimiyya kwa ajili ya kupaki magari na kuyasafisha pamoja na kuweka mafuta, aidha sehemu hiyo ilitumika kama mahala pa kupumzikia madereva waajiriwa na wanao jitolea, hali kadhalika tulitengeneza gereji inayo hamishika kwa ajili ya kutengeneza gari lolote litakalo haribika wakati wowote na mahala popote, sambamba na kuandaa madereva wa hakiba kwa ajili ya kumpokea dereva yeyote atakaepatwa na tatizo –Allah atuepushie- wakati wowote”.
Akabainisha kua: “Hali kadhalika tumeandaa magari ya kutoa huduma maalum, kama vile magari ya wagonjwa na magari ya kugawa maji pamoja na magari yanayo toa huduma ya kwanza kwa wagonjwa”.
Akasisitiza kua: “Kazi imefanyika saa (24) kila siku na itaendelea hadi zaairu wa mwisho atakapo ondoka Karbala”.