Maukibu ya kuomboleza: Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji chashirikiana na waumini katika kuhuisha ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kupitia wawakilishi wake kutoka mikoa tofauti ya Iraq, Adhuhuri ya siku ya Jumamosi (20 Safar 1441h) sawa na (19 Oktoba 2019m) kimeungana na mamilioni ya watu wanaokuja Karbala, kupitia maukibu ya kuomboleza kwa ajili ya kuhuisha ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Katika maukibu hiyo imeshiriki idadi kubwa ya makamanda wakiongozwa na mkuu wa kikosi hicho Ustadh Maitham Zaidi, maukibu iliingia katika haram ya bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein (a.s) na kuhuisha kiapo cha utii kwake pamoja na kumpa pole Imamu Hujjat bun Hassan Almuntadhir (a.f), na kuwakumbuka ndugu zao mashahidi walio uwawa kwa ajili ya kulinda taifa hili tukufu pamaja na maeneo matakatifu, kisha wakakatisha uwanja wa katikati ya haram mbili huku wakiimba kaswida za kuomboleza na kuonyesha mapenzi yao kwa baba wa watu huru -Abul-Ahraar- (a.s).

Halafu maukibu ikaingia katika haram tukufu ya Abbasi kisha kiongozi mkuu wa kikosi Ustadh Maitham Zaidi akaongea, alianza kwa kumshukuru kila mtu aliye jitolea kufanikisha ziara hii kutoka mikoa tofauti ya Iraq, kwa kutoa huduma za aina mbalimbali kwa mazuwaru watukufu, baada ya mada yake ikafuata majlisi ya matam ambayo mazuwaru walio kuwepo ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pia wakashiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: