maahadi ya Qur’ani tukufu kitengo cha wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kuhitimisha harakati zake katika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) 1441h.
harakati hizo zilidumu kwa muda wa wiki mbili, matawi yote ya maahadi yalishiriki, vituo vyake viliwekwa kwenye barabara zote zinazo elekea Karbala, walikua wanafundisha usomaji sahihi wa surat Fat-ha pamoja na kuelezea baadhi ya mafundisho ya Qur’ani tukufu na baadhi ya hukumu za ziara ya Arubaini na utukufu wake, pamoja na namna ya kumuiga bibi Hauraa (a.s) na lengo la kuhuishwa kwa ziara hii, sambamba na jinsi ya kufaidika na wakati kwa kufanywa istighfaar na kuomba dua, pia waliweka mashidhano madogo madogo na kutoa zawadi kwa washindi.
Kumbuka kua Maahadi ya Qur’ani tukufu kitengo cha wanawake ni moja ya miradi muhimu ya kielimu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inamiradi mingi ndani ya kipindi chote cha mwaka kwenye mikoa tofauti ya Iraq.