Ugeni wa wizara ya habari na utamaduni umepongeza mafanikio ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyesho ya kimataifa yanayo fanyika mjini Frankfud ya mwaka 2019.

Maoni katika picha
Mazungumzo kati ya ugeni wa wizara ya habari ya Ujerumani na mwakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa Ulaya Sayyid Ahmadi Ridhwa Husseini, miongoni mwa wageni muhimu walio tembelea tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu linalo shiriki katika maonyesho ya vitabu huko Frankfud Ujerumani wanatoka wizara ya habari na utamaduni.

Ustadh Harith Rashidi kutoka wizara ya habari ya Ujerumani amesifu harakati za kielimu zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu na umuhimu wa ushiriki wao kwenye maonyesho hayo.

Huku Ustadh Shadhaan Abdullah Ramhi kutoka wizara hiyo hiyo akisifu ushiriki wa Iraq kwa ujumla kupitia taasisi mbalimbali, zikiongozwa na Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: