Haya ndio yaliyo fanywa na Masayyid wanao fanya kazi katika Atabatu Abbasiyya tukufu siku za ziara ya Arubaini na baada yake

Maoni katika picha
Kama kawaida yao katika kila mwaka, Masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya wamekua wakitoa huduma kwa mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), na wameenea ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na maeneo yote ya mazuwaru ndani ya mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kutoa huduma, utawakuta wanashindana katika kutoa huduma bila kuchagua hadi huduma ndogo kabisa.

Hawaja jikita katika huduma za aina moja peke yake, ukizingatia kua sio wengi kwa idadi ukilinganisha na watu wengine, wapo ndani ya haram tukufu wanasaidia kuongoza matembezi ya mawakibu na mazuwaru, wanafanya usafi muda wote ndani ya haram hiyo, wanatandua miswala wakati mawakibu zinapo ingia na kuitandika wakati wa swala za jamaa.

Mtandao wa kimataifa Alkafeel umefanya mazungumzo na kiongozi wa idara hiyo Sayyid Hashim Shaani ambaye ametuambia kwa ufupi kazi zinazo fanywa na Idara yake wakati wa ziara ya Arubaini na baada yake, amesema kua: “Kitengo chetu ni sawa na vitengo vingine vya Ataba tukufu, idara ya Masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya imetoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru, na hiyo ndio kawaida yetu kila mwaka, miongoni mwa huduma tulizo toa ni:

  • 1- Tumesaidia kazi ya kugawa chakula katika migahawa ya Atabatu Abbasiyya tukufu (mgahawa na ndani ya Ataba, maukibu Ummul Banina katika barabara ya Najafu, mgahawa na mji wa mazuwaru wa Alqami katika barabara ya Hilla na mgahawa wa Shekh Kuleini katika barabara ya Bagdad), tumegawa chakula, maji na chai kwa mazuwaru kipindi chote cha ziara, mazaairu hupokea huduma wanazo pewa na Masayyid waliovaa ngua maalum, wana nafasi kubwa ya kuathiri nafsi za mazuwaru, sambamba na maneno mazuri wanayo tumia katika kuwakaribisha mazuwaru hao.
  • 2- Tumesaidia kupokea mazuwaru ndani ya Ataba na kuongoza matembezi yao pamoja na mawakibu za kuomboleza.
  • 3- Tumesaidia kudumisha usafi ndani ya haram na kwenye milango ya Ataba tukufu, kwa kutandua kufanya usafi na kutandika miswala pamoja na kuweka misahafu na vitabu vya ziara sambamba na kuweka turba za kutosha.
  • 4- Tumegawa maelfu ya nakala za ziara ya Arubaini kwa mazuwaru watukufu ndani ya haram.
  • 5- Kuondoa vitambaa vinavyo tupwa juu ya kaburi tukufu na kuvikabidhi katika kitengo cha zawadi na nadhiri.
  • 6- Tumesaidia kupokea mawakibu na kuongoza uingiaji wao na utokaji ndani ya haram tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: