Mazuwaru wa Arubaini waliobaki wanaendelea kuhudumiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu: mwaka wa tatu mfululizo mazuwaru wa kigeni wanawasili Karbala baada ya mwezi ishirini Safar

Maoni katika picha
Pamoja na kutofika kwao kwa wakati kwenye ziara tukufu ya Arubaini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao, idadi kubwa ya mazuwaru kutoka Pakistani, Afghanistani, India na wengine kutoka Asia na Ulaya pamoja na Lebanon na Sirya, wamewasili Karbala kwa kuchelewa na kufanya ziara ya Arubaini, kwa sababu tofauti, ikiwa ni pamoja na mazingira ya hali ya hewa na kuchelewa kupata ruhusa ya kuingia Iraq kwa ajili ya ziara ya Arubaini, hali hii imejirudia kwa mwaka wa tatu mfululizo.

Pindi wanapo wasili Karbala wanaikuta Atabatu Abbasiyya tukufu imewaandalia kila wanacho hitaji, kwa ajili ya kuwafanyia wepesi ukaaji wao na utendaji wa ibada zao, Ataba tukufu imeweka maelfu ya matandiko ndani ya Sardabu na kuweka mazingira mazuri ya kulala pamoja na sehemu zingine zilizo chini yake nje ya haram tukufu, hali kadhalika mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) umejaa vyakula kwa ajili ya mazuwaru hawa wanaofika baada ya kipindi cha ziara ya Arubaini, aidha imeweka utaratibu mzuri wa kuingia na kutoka katika eneo lenye kaburi tukufu bila usumbufu wowote, hadi katika matembezi yao ndani ya mji mtukufu wa Karbala.

Fahamu kua maelfu ya mazuwaru wa kigeni wanawasili Karbala kufanya ziara ya Arubaini baada ya siku hiyo kupita, kama kawaida yake Ataba tukufu haijabaki nyuma katika kutoa huduma kwa kila anaye kuja kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: