Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji chakamilisha kazi yake ya kulinda amani na kutoa huduma katika ziara ya Arubaini ya mwaka 1441h kwa mafanikio…

Maoni katika picha
Viongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwa/26 Hashdi Shaábi), wamekamilisha kazi ya ulinzi na utowaji wa huduma kwa mazuwaru waliokuja Karbala kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) mwaka huu 1441h.

Mkuu wa kikosi hicho Ustadh Maitham Zaidi amesema kua: “Kazi hii imefanywa na zaidi ya skari (5500) jukumu letu lilikua chini ya mkakati maalum uliopangwa na makamanda wa jeshi”.

Akabainisha kua: “Kikosi kilisimamia ulinzi katika malango matatu ya kuingia Karbala (kaskazini upande wa Bagdad, mashariki upande wa Hilla na kusini upande wa Najafu), wameingia zaidi ya mazuwaru milioni kumi kupitia vituo vyetu vya ukaguzi, ni fahari kubwa kwetu kuhudumia idadi kubwa ya wapenzi wa kaaba ya uhuru”.

Akasema: “Kuwepo kwa ushirikiano wa juu kati ya kikosi chetu na makamanda wa hashdi Shaábi pamoja na mkakati uliotekelezwa kwa ufanisi mkubwa, ushiriki wa kikosi ni kielelezo cha uwiyano wa bwana wa mashahidi (a.s) na mafundisho ya Ahlulbait (a.s), kwani sisi ni tunda la mpinduzi matukufu ya Ashura”.

Naye makamo kiongozi mkuu wa kikosi Sayyid Haidari Mussawi akasema: “Hakika kikosi hiki jukumu lake ni kuimarisha ulinzi na usalama, na kutoa huduma kwa mazuwaru kama usafiri, chakula, vinywaji pamoja na matibabu, sambamba na kuratibu matembezi ya mazuwaru na mawakibu za waombolezaji”. Akaongeza kua: “Kazi zetu huboreshwa kila wakati, mwaka huu yumewaandalia sehemu za kulala na kupumzika mazuwaru pamoja na kuwawekea kila kitu kinacho hitajika”.

Mussawi akasema: “Hakika kikosi hiki mwishoni mwa ziara, mwezi ishirini safar kimeratibu matembezi ya kuomboleza kwa ajili ya kula kiapo upya kwa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuahidi kua kitaendelea kutoa huduma kwa wapenzi na wafuasi wake kila mwaka kwa idhini ya Mwenyezi Mungu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: