Idara ya intanet chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza maboresho ya App ya (Haqibatu Mu-uminu) inayo patikana kwenye simu za kisasa (smart phone) zenye program ya (IOS) kwa ajili ya kurahisisha upakuaji.
Wataalamu wetu wa ofisi ya maboresho chini ya idara ya intanet wamefuta App ya zamani na kuweka mpya kwa ajili ya kuepusha usumbufu na kutoa fursa ya kunufaika zaidi kwa watumiaji wa App ya (Haqibatu Mu-uminu).