Kitengo cha Dini kimetangaza kufanikiwa kwa mkakati wake katika ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kufanikiwa mkakati wake katika ziara ya Arubini kwenye sekta ya tblighi utamaduni na maelekezo, kimesema kua maelfu ya mazuwaru wamefaidika na kitengo hicho, kupitia vituo walivyo fungua kwenye barabara zinazo elekea Karbala na ndani ya haram tukufu, pamoja na kwenye majengo ya kutoa huduma chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu na mawakibu za kutoa huduma.

Kitengo kimefafanua kua:

  • - Kilifungua vituo vya tabligh kwa ajili ya kujibu maswali ya mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) chini ya utaratibu wa tablighi za kihauza.
  • - Tumegawa maelfu ya vipeperushi kwa mazuwaru vyenye mafundisho na maelekezo mbalimbali.
  • - Kusimamia swala za jamaa katika majengo ya kutoa huduma yaliyo chini ya Atabatu Abbasiyya pamoja na ndani ya ukumbi wa haram tukufu.
  • - Kujibu maswali ya mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ofisi ya kitengo muda wote.
  • - Kutoa mawaidha ndani ya ukumbi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na katika barabara zinazo tumiwa na mazuwaru wengi.
  • - Kupeleka mubalighina katika mawakibu za kutoa huduma kwa ajili ya kusaidia kutoa maelekezo na mawaidha.
  • - Kuendesha vipindi kwenye luninga na redio vinavyo fafanua malengo ya zira ya Arubaini.
  • - Kuweka hadithi zinazo zungumzia ziara ya Arubaini kwenye mabango yaliyopo ndani na nje ya haram tukufu.
  • - Kuweka matangazo yanayo elekeza badhi ya mambo muhimu kwa mazuwaru, sehemu nyingine ya vipeperusi vinaeleza adabu na malengo ya ziara.

Fahamu kua kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu ni miongoni mwa vitengo vyenye mafungamano ya moja kwa moja na mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s), kwani kinajukumu la kuwaongoza mazuwaru kiroho na kuwafafanulia malengo ya ziara, kwa kueleza kila kitu kikubwa na kidogo, na kumfanya zaairu atambue mambo aliyo kusudia Imamu Hussein (a.s), na kuwafanya walimwengu waweze kuyafanyia kazi kwa kupambana na dhulma kila sehemu ya dunia, sio wafuasi wa Ahlulbait (a.s) peke yake, bali kwa waumini wa Dini zote, na hayo ndio makusudio ya mapinduzi ya Husseiniyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: