Kitu gani alichosema waziri wa utamaduni na michezo wa Qatari kuhusu machapisho ya Atabatu Abbasiyya tukufu?

Maoni katika picha
Ustadh Ibrahim Sayyid mshauri wa waziri wa utamaduni na michezo wa Qatari na mkuu wa kongamano la wasambazaji, amesifu harakati za kitamaduni na kielimu zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, na maendeleo makubwa waliyo pata katika miradi ya kitamaduni, amesema hayo baada ya kutembelea tawi la Atabatu Abbasiyya linalo shiriki kwenye maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayo fanyika mjini Frankfut Ujerumani.

Muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu barani Ulaya Sayyid Ahmadi Raadhi Husseini alipo tembelewa na Ustadh Ibrahim na baada ya ulizwa harakati hizi zinaumri gani, akasema: “Asilimia kubwa ya miradi ya utamaduni na uandishi katika Ataba tukufu imeanza baada ya kuanguka utawala wa kidikteta (9/4/2003m), kabla ha hapo kulikua na miradi michache sana iliyo anzishwa kabla ya kuingia utawala huo mwaka (1968m) ilikua imesimama kwa muda wa miaka (35) ya utawala wa kidikteta ulio angamiza mashamba na vizazi, baadhi ya harakati sio kwamba zilifungwa tu mwaka wa (1968m) bali zilifungwa na kuhujumiwa, kwa mfano maktaba kuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu iliyo anzishwa mwaka (1964m)”.

Akafafanua kua: Uongozi mpya wa kisheria chini ya Marjaa Dini mkuu katika mji mtukufu wa Naafu, umefanikiwa kurudisha maktaba na kuiendeleza kwa kuweka maelfu ya vitabu vya aina mbalimbali, bali wameongeza kitengo cha faharasi, uandishi na uhakiki wa nakala kale, sambamba na kuweka maktaba ya kielektronik na ofisi ya masomo ya juu kwenye vyuo vikuu vya Iraq, maktaba hii sasa inapewa nafasi ya pili kieneo, imeendelea kwenye sekta tofauti”.

Sayyid Raadhi akaendelea kusema kua: “Tumesha fanya makumi ya miradi ya kitamaduni na kufungua taasisi kwa ajili ya kuendesha miradi hiyo, kama vile vituo vya uandishi, utafiti, uhakiki, tarjama, makongamano, filamu na matangazo mubashara na mingineyo miongoni mwa miradi iliyotoa matunda mazuri katika sekta tofauti, kama vile uendeshaji wa semina, majarida ya watoto, vijana wa kiume na wakike, redio ya wanawake, kituo cha uzalishaji Alkafeel, wamerudisha harakati zote za kitamaduni zilizo kua zimesimama tangu mwaka (1968m) wakati wa utawala wa kidikteta uliopita”.

Akabainish kua: “Miradi ya kitamaduni na kielimu iliyo fanywa baada ya kuanguka utawala wa kidikteta ndani ya miaka hii ni zaidi ya mara mia ya miradi yote yaliyo fanywa katika umri wa Ataba tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: