Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kitengo ch malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya kimetangaza kuanza usajili katika michepuo yake ya (Udaktari – Uuguzi – Udaktari wa meno) kwa mwaka wa masomo 2019 – 2020, wamesema kua mwanafunzi anaweza kwenda kupata maelekezo chuo kikuu cha Karbala au kwenye vituo vya maelekezo vilivyo karibu yake katika mikoa mingine, pamoja na vielelezo vyake kama vilivyo tajwa kwenye kipeperushi, awe na namba ya mtihani na matokeo yake ya mtihani kutoka kwenye shule aliyo somea, kisha atume kwenye linki ifuatayo: https://pe-gate.org
Kwa maelezo zaidi fika chuoni mjini Karbala/ barabara ya Karbala – Najafu/ mkabala na nguzo namba (1238) au piga simu katika namba zifuatazo: (07817448000 / 07733078000 / 07602418000).