Kazi kubwa ya usafi inafanywa ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kutandika miswala.

Maoni katika picha
Baada ya kuisha msimu wa ziara ya Arubaini, mazuwaru wameanza kupungua siku baada ya siku, watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanaofanya kazi katika kitengo cha uangalizi wa haram tukufu pamoja na vitengo vingine, wameanza kusafisha ukumbi wa haram tukufu.

Katika kazi hiyo pia wameshiriki mazuwaru, wametandua kapeti zilizo tandikwa karibu na kipindi cha ziara na kupiga deki halafu wakatandika mazulia yaliyo kuwepo awali baada ya kuyasafisha.

Kazi hiyo imekua ikifanywa katikati ya usiku kwa ajili ya kuepuka kuwasumbua mazuwaru na kupata nafasi ya kufanya kazi kwa uhuru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: