Idara ya shule za Dini Alkafeel za wasichana: Tuliongeza huduma zetu katika ziara ya Arubaini na kufaidisha maelfu ya mazuwaru

Maoni katika picha
Idara ya shule za Dini Alkafeel za wasichana katika Atabatu Abbasiyya imesema kua, imefanikiwa katika mkakati wake wa kutoa huduma kwenye ziara ya Arubaini, kwa kutoa huduma nyingi za maelekezo, mafundisho ya Dini na matibabu, huduma zote zimeboreshwa mwaka huu, sambamba na kuongezeka idadi ya wanufaika, ambao ni maelfu ya mazuwaru, watumishi wetu walikua zaidi ya (350) ambao ni walimu wa shule pamoja na wanafunzi wa vyuo waliopata semina maalumu na mafunzo ya Skaut siku za nyuma.

Kwa mujibu wa maelezo ya bibi Bushra Kinani kiongozi wa idara ya shule za Dini Alkafeel, amesema: “Kila mwaka huja kwako mamilioni ya nyoyo, hauko peke yako ewe Abu Abdillahi, wafuasi wako na wapenzi wako hukujia kutoka kila sehemu ya dunia wakiwa wamebeba pendera yako na kusema (laiti tungeku pamoja na wewe kiongozi wetu), kila mwaka Karbala hua hai kwenye nyoyo za wapenzi wako katika kukumbuka ushujaa na msimamo wako, kila mwaka huja mabinti wa Zaharaa (a.s) kutoka idara ya shule za Dini Alkafeel katika ziara ya Arubaini, wanaitikia wito wa utukufu wa kutoa huduma kwa mazuwaru na kumliwaza bibi Zainabu Hauraa (a.s)”.

Akasema: “Tulikua na zaidi ya watumishi (350) walimu wa kike na wanafunzi wa shule zifuatazo: Fatuma binti Asadi (a.s) shule ya Quráni na msomo ya Dini/ Karbala tukufu, Nuuru Zaharaa/ Bagdad, Zainabu binti Ali (a.s)/ Bagdad, Rihanatul Mustwafa (a.s)/ Bagdad, Ummu Sibtaini (a.s)/ Bagdad, Ummul Banina (a.s) Diwaniyya, Ummu Abiiha (a.s)/ Najafu, Albatuli (a.s)/ Muthanna, Hauraa (a.s)/ Muthanna, Al-Aqiilah (a.s)/ Dhiqaar, Al-Ilmu/ Basra, Darul-Ilmu katika mkoa wa Nafafu chini ya idara ya shule za Dini Alkafeel za wasichana, sambamba na wanafunzi wa vyuo mbalimbali waliopata mafunzo katika kambi za Skaut za majira ya kiangazi zinazo endeshwa na idara hii kwa wanafunzi wa vyuo”.

Huduma walizokua wanatoa kwa mujibu wa maelezo ya Kinani ni: “Matibabu, tablighi, kujibu maswali ya kifiqhi, kuendesha ratiba maalum ya Quráni kwa watoto waliokuja katika ziara hii, kukaribisha wageni na kuwapa huduma muhimu katika maeneo yafuatayo: (Jengo la Shekh Kuleini – jengo la Alqami, mgahawa wa nje chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu – Jengo la Ummul Banina (a.s) – Haram tukufu ya Abbasi), nyoyo zao zilikua zikiongea na moyo wa Hauraa pamoja na Batuli (a.s) zikisema (Mwenyezi Mungu ayakuze malipo yako kiongozi wangu kwa kumbukumbu ya Arubaini ya bwana wa vijana wa peponi).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: