Atabatu Abbasiyya tukufu yajiandaa kuomboleza na kutoa huduma katika kumbukumbu ya kifo cha Mtume (s.a.w.w).

Maoni katika picha
Huzuni kubwa inakutana na huzuni iliyokuwepo katika Atabatu Abbasiyya siku zilizo pita, waislamu wanapokea moja ya matukio makubwa, nalo ni kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), Ataba tukufu imewekwa upya mapambo meusi yaliyo andikwa ujumbe unao ashiria huzuni kutokana na kifo cha mbora wa walimwengu Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Kama kawaida katika tukio hili la kuhuzunisha, Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum ya kuomboleza yenye mambo yafuatayo:

  • 1- Kufanya majlisi za kuomboleza ndani ya haram tukufu ya Abbasi kwa ushiriki wa mazuwaru watukufu watakao kuja kuomboleza msiba huu.
  • 2- Kupokea mawakibu za kuomboleza zitakazo anza matembezi yao kutokea mji mkongwe na barabara zingine za Karbala kwa ajili ya kumpa pole Imamu Mahadi msubiriwa (a.f) kwa kufiwa na babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w).
  • 3- Kufanya majlisi rasmi ya kuomboleza kwa ajili ya wafanyakazi wa Atabatu Abbasiyya tukufu ndani ya ukumbi wa utawala.
  • 4- Kufanya matembezi (maukibu) ya kuomboleza kwa pamoja kati ya Atabatu Husseiniyya na Abbasiyya baada ya Adhuhuri ya (28 Safar), kwa ajili ya kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kutokana na msiba huu.
  • 5- Kufungua mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na madirisha yake ya nje pamoja na ukumbi wake mkuu wa ndani ya haram tukufu kwa ajili ya kugawa chakula kwa mazuwaru watakao kuja Karbala kuomboleza kifo cha Mtume (s.a.w.w).

Kukumbuka kua kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) kilitokea mwezi 28 Safar mwaka wa 11 hijiriyya, wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) huenda katika kaburi la simba wa Mwenyezi Mungu Ali bun Abu Twalib (a.s) katika mji wa Najafu, kumpa pole na kumliwaza kwa kifo cha ndugu yake mtoto wa Ammi yake Mtume wa rehema Muhammad (s.a.w.w) nao ni miongoni mwa misimu ya ziara maalum.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: