Masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wanaomboleza kifo cha babu yao Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w).

Maoni katika picha
Kama kawaida yao katika kukumbuka misiba ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), idara ya masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi maalum kwa ajili ya kuomboleza msiba wa kifo cha babu yao Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na kuwapa pole waislamu wote.

Majlisi hiyo imefanywa ndani ya haram ya Abbasi na kuhudhuriwa na kundi kubwa la waumini waliokuwepo ndani ya haram hiyo, mzungumzaji alikua ni Shekh Ali Muhani kutoka kitengo cha Dini, akaelezea kuhusu uhai wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambao ndio muongozo wa kila muislamu anayetaka ukamilifu na mafanikio, pia akaelezea kifo cha Mtume (s.a.w.w) na namna waislamu wanavyo athirika na msiba huu.

Majlisi ikahitimishwa kwa kusomwa kaswida zinazo unyesha ukubwa wa huzuni iliyopo katika nyoyo za waislamu, ukizingatia msiba huu ni pigo kubwa kwa kila muislamu kote duniani.

Kumbuka kua kifo cha Mtume Muhammad bun Abdillahi (s.a.w.w) kilitokea mwezi (28) Safar mwaka 11 hijiyya akiwa na umri wa miaka 63, wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait huelekea kwenye kaburi la simba wa Mwenyezi Mungu Ali bun Abu Twalib (a.s) katika mji wa Najafu, kwenda kumpa pole kwa kifo cha ndugu yake na mtoto wa ammi yake Mtume Muhammad (s.a.w.w), nayo ni miongoni mwa ziara maalum.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: