Mamilioni ya waumini kutoka ndani na nje ya Iraq wamekuja kuomboleza kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika kaburi la mtoto wa Ammi yake na wasii wake Ali bun Abu Twalib (a.s), huku huduma zikiboreshwa na ulinzi ukiimarishwa na Atabatu Alawiyya tukufu kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kutoka mkoani.
Asilimia kubwa ya mazuwaru waliokuja kutoka mikoani wametembea kwa miguu, wakiwa na nia thabiti ya kuomboleza msiba buu kwa zaidi ya siku tatu, mawakibu za kutoa huduma zimeenea kwenye barabara zote zinazo elekea katika malalo tukufu ya Imamu Ali (a.s), katika maombolezo haya wairaq wameshirikiana na mazuwaru wengi wa kigeni ambao bado hawajaondoka tangu walipokuja kwa ajili ya ziara ya Arubaini iliyo fanyika mwanzoni mwa wiki iliyo pita.
Kumbuka kua miongoni mwa mambo bora yaliyo tajwa katika riwaya za watu wa nyumba ya Mtume (a.s) ni kumzuru kiongozi wa waumini (a.s) katika msiba huu.