Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanampa pole Imamu Hussein (a.s) katika kumbukumbu ya kifo cha babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w).

Maoni katika picha
Kwa majonzi na huzuni kubwa, baada ya Adhuhuri ya leo (28 Safar 1441h) sawa na (27 Oktoba 2019m) watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wamefanya matembezi ya kuomboleza kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kumpa pole Imamu Hujjat bun Hassan (a.f) pamoja na bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Matembezi yameanzia katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) baada ya kusimama na kutoa pole kwa mwenye malalo hiyo takatifu, kisha wakaanza kutembea wakielekea katika malalo ya Abu Abdillahi Hussein (a.s), kwa kupitia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu huku wakipiga matam na kuimba mimbo ya kuomboleza kifo cha mbora wa walimwengu, walipofika katika malalo ya baba wa watu huru (a.s) wakapokewa na ndugu zao watumishi wa Atabatu Husseiniyya tukufu na wakaungana nao katika kuomboleza, kisha wakafanya majlisi ya pamoja ambayo mazuwaru wengi waliokua ndani ya malalo hiyo wakashiriki.

Fahamu kua Atabatu Abbasiyya tukufu iliandaa ratiba maalum ya kuomboleza msiba huu mkubwa kwa waumini wote duniani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: