Kwa ushiriki wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya: Maukibu ya watu wa Karbala yaomboleza kifo cha Mtume katika kaburi la Imamu Ali (a.s).

Maoni katika picha
Kwa ushiriki wa Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya kupitia kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya, imewasili katika mji mtukufu wa Najafu maukibu ya pamoja ya watu wa Karbala kuomboleza kifo cha Mtume Muhammad bun Abdullahi (s.a.w.w) na kumpa pole ndugu yake, khalifa wake, wasii wake, kiongozi wa waumini (a.s), na kuhuisha ahadi ya kushikamana na mafundisho pamoja na mwenendo wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Wamefanya majlisi ya kuomboleza ndani ya haram ya Alawiyya, iliyo pambwa na kaswida pamoja na tenzi zilizo amsha hisia za uchungu wa msiba huo, wakati wa matembezi ya maukibu hiyo washiriki wameimba kaswida na mashairi yaliyo onyesha ukubwa wa msiba huu.

Rais wa kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Maukibu ya kuomboleza ya watu wa Karbala na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimezowea kushirikiana nayo katika kila tukio, hufanya nao mikutano mara kwa mara katika mkoa wa Karbala, kwa ajili ya kuhakikisha wanafanya uombolezaji katika hali nzuri, inayo endana na utukufu wa kumbukumbu hii sambamba na heshima ya Karbala tukufu”.

Akaongeza kua: “Tuliandaa magari kadhaa kutoka kitengo cha usafirishaji cha Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kubeba waombolezaji kutoka Karbala kuja Najafu na kuwarudisha, pamoja na kuandaa baadhi ya mahitaji ya maukibu”.

Kumbuka kua hii hufanywa kila mwaka na watu wa Karbala kwa ajili ya kuomboleza matukio ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), maukibu hii inaundwa na mawakibu tofauti pamoja na vikundi vya Husseiniyya vya watu wa Karbala pamoja na wakazi wa mji huo mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: