Maahadi ya Quráni tukufu yahitimisha mradi wa kufundisha usomaji sahihi wa Quráni kwa mazuwaru wa kiongozi wa waumini (a.s).

Maoni katika picha
Baada ya mafanikio yaliyo patikana katika vituo vya kufundisha usomaji sahihi wa Quráni kwa mazuwaru wa ziara ya Arubaini, leo Maahadi ya Quráni kupitia tawi lake la Najafu inahitimisha mradi wa (kufundisha usomaji sahihi kwa mazuwaru) wa kiongozi wa waumini (a.s) katika kumbukumbu ya kifo cha Mtume (s.a.w.w).

Ofisi ya Maahadi imesema kua ileweka vituo vyake kwenye barabara zote zinazo elekea haram, hasa zile zenye watu wengi, ili kunufaika na ziara hii, vituo vimepata muitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru, wameonyesha moyo wa kupenda kujifunza usomaji sahihi wa Quráni hasa sura fupi wanazo tumia katika swala za faradhi za kila siku pamoja na nyeradi zake.

Tawi la Maahadi katika mji wa Nafafu limefanya kila kitu kwa ajili ya kufanikisha awamu ya tatu ya mradi huu, baada ya kupewa na Atabatu Abbasiyya kila kinacho hitajika, nayo ni fursa nzuri ya kufundisha usomaji sahihi wa Quráni na nyeradi za swala vitu ambavyo ni sharti la kusihi kwa swala.

Mazuwaru wameishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia Maahadi ya Quráni kwa kufanya mradi huu muhimu, wa kufundisha usomaji sahihi wa Quráni pamoja na nyeradi za swala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: