Amani ewe Iraq ya mawalii: Ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) watumishi wameliombea taifa la Iraq na raia wake amani na usalama.

Maoni katika picha
Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) hawaja sahau changamoto na matatizo yanayo likumba taifa la Iraq kwa sasa, watumishi hao wamefanya tukio la kiibada Adhuhuri ya Jumatatu (29 Safar 1441h) sawa na (28 Oktoba 2019m) ndani ya haram takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) mbele ya malalo yake tukufu wakaomba na kusoma tawasul kwa unyenyekevu mkubwa wakimuomba Mwenyezi Mungu alinde taifa la Iraq na alipe amani na utulivu.

Baada ya kusoma ziara maalum ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuimba wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu (Lahnul-Ibaa), walianza kuimba kaswida zinazo eleza hali ya taifa la Iraq kwa sasa, wakamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu kwa kutawasal na huyu wanaye mtumikia, awape utulivu na amani raia wote wa Iraq, na awaepushe na shari ya fitna pamoja na kuwalinda vijana wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: