Viongozi wa wahariri wa jarida hilo wamesema kua tumeongeza muda kutokana na mahitaji ya watafiti na kutoa nafasi ya kupata idadi kubwa zaidi ya washiriki, mwisho wa kupokea tafiti hizo ni tarehe (15/2/2020m) badala ya (1/12/1019m) na matokeo yatatangazwa tarehe (1/4/2020m).
Wakasisitiza kua masharti ya mashindano yamebaki kama yalivyo kua:
- Tafiti zijikite katika fani mbili kuu za jarida (Uhandisi na Udaktari).
- Tafiti isiwe imesha tangazwa au kutolewa na watu wengine.
- Tafiti iandikwe kwa lugha ya kiengereza.
- Tafiti ikidhi vigezo vya jarida, iwe inafaa kuwekwa kwenye mtandao maalum wa jarida.
- Utafiti utakao kubaliwa kushiriki katika shindano, mtafiti atatakiwa kuahidi kufuata kanuni za utangazaji wa jarida la Albaahir sawa awe alishinda zawadi au hakushinda.
- Mshindi wa kwanza atapewa dola 800/ wa pili dala 600/ na wa tatu dola 400.