Hospitali ya rufaa Alkfeel chini ya Atabtu Abbasiyya tukufu imetoa ufafanuzi na kujibu uzushi wa baadhi ya mitandao ya kijamii, ifuatayo ni nakala yake:
Hospitali ya rufaa Alkafeel ilifungua milango yake tangu siku ya kwanza ya maandamno yanayo shuhudiwa hapa Iraq, imekua ikipokea watu waliojeruhiwa kwenye maandamano hayo raia na askari, tambueni kua hospitali inafanya kila iwezalo katika mazingira haya ambayo taifa letu linapitia, inatoa bure huduma zote za matibabu kwa waathirika wa maandamano, kama ilivyo fanya kwa waathirika wa matukio mbalimbali ya Karbala, likiwepo tukio la ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).
Tunawajulisha wairaq wote kua Hospitali ya rufaa Alkafeel itaendelea kuonyesha uzalendo, haita acha kusaidia raia wa Iraq wakati wowote wanapo pata majanga.
Tambua kua baadhi ya mitandao ya kijamii inayo chochea fitna imezusha kua hospitali ya Alkafeel imekataa kupokea watu wanao jeruhiwa kwenye maandamano na kuwafukuza, habari hiyo sio ya kweli kabisa.