Mwezi mtukufu wa Rabiul-Awwal unamambo ya kihistoria yaliyo tokea katika umma wa kiislamu, miongoni mwa matukio hayo ni kulala kwa Imamu Ali (a.s) katika kitanda cha Mtume (s.a.w.w), usiku wa kwanza wa mwezi huu mwaka wa (13) wa utume, tukio hilo linaonyesha ushujaa wa kiongozi wa waumini Ali (a.s).
Historia haijasimulia kisa kinacho sisimua zaidi ya hiki, makuraishi walipanga kumuua Mtume Muhammad akiwa amelala kwenye kitanda chake, Mtume (s.a.w.w) akatambua njama hiyo na akamuambia Ali, akalia kwa kuogopa kuuwawa kwa Mtume, lakini alipo ambiwa na Mtume alale yeye katika kitanda hicho, akasema: nikilala mimi na kukulinda kwa nafsi yangu utasalimika?! Mtume (s.a.w.w) akasema: ndio, hivyo ndio alivyo niahidi Mola wangu, Ali akafurahi sana alipo jua kua Mtume atasalimika, akaenda kitandani na akalala akiwa roho yake imetulia kabisa na akajifunika shuka.
Ali (a.s) alilala katika kitanda cha Mtume (s.a.w.w) akiwa amejitolea kufa, makuraishi wakaja kutaka kutekeleza njama yao, walipo taka kumshambulia huku wakiwa wanajua aliye lala pale ni Muhammad (s.a.w.w), walimuona usoni kwake na wakatambua sio Mtume, ndipo wakaondoka kwenda kumtafuta Mtume (s.a.w.w).
Kiongozi wa waumini Ali (a.s) alitilia umuhimu mkubwa swala la kutangaza Dini ya kiislamu, lilionekana hilo kwake kutokana na utayari wake wa kujitolea na kumsaidia Mtume (s.a.w.w) kwenye vita na maeneo mengine kama ilivyo kuja katika historia.
Kulala kwa kiongozi wa waumini Ali (a.s) katika kitanda cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) halikua jambo dogo linalo weza kufanywa na mtu yeyote, ni jambo linalo hitaji ushujaa mkubwa, ukizingatia kua alikua anajua lazima atauwawa, kwa sabbu makurishi walikua wamepanga kuangamiza Dini na kumuua Mtume katika usiku huo, Mtume (s.a.w.w) aliondoka bila kuonekana na mtu yeyote huku anasoma maneno ya Mwenyezi Mungu yasemayo: (Tumeweka kizuwizi mbele yao, na kizuwizi nyuma yao, na tumefunika macho yao; kwa hivyo hawaoni), huku akimuacha kiongozi wa waumini akiwa amelala kwenye kitanda chake na kuthibitisha maneno ya Mwenyezi Mungu yasemayo: (Na katika watu yupo ambaye huiuza nafsi yake kwa kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni mpole kwa waja wake).