Kurudisha bendera nyekundu katika kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maoni katika picha
Baada ya swala ya Isha siku ya Jumanne (30 Sarar 1441h) sawa na (29 Oktoba 2019m) imebadilishwa bendera nyeusi ya kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuwekwa bendera nyekundu, kama ishara ya kumaliza msimu wa huzuni uliodumu miezi miwili, Muharam na Safar, na tangazo la kuingia mwezi wa Rabiul-Awaal.

Fahamu kua bendera nyekundu hupepea juu ya kubba hilo takatifu kwa muda wa miezi 10, inaonyesha kua mwenye kaburi hili aliuwawa na bado kisasi chake hakija lipwa, zamani waarabu alikua anapo uwawa mtu wanaweka bendera nyekundu juu ya kaburi lake, haiondolewi hadi watakapo lipa kisasi, hadi leo bado bendera nyekundu hazija tolewa kwenye kubba la malalo ya bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mtu anaweza kuuliza mbona mwezi wa Muharam na Safar hatuoni bendera nyekundu bali tunaona nyeusi? Jibu ni kwamba: bendera nyeusi inaonyesha kua katika siku kama hizi ndio alizo uwawa mwenye kaburi hili, ndio maana hua inawekwa bendera nyeusi kwenye kubba la malalo ya bwana wa mashahidi Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Ewe kiongozi wetu ewe Imamu wa zama haujafika wakati wa kulipa kisasi cha watu walio uwawa katika ardhi ya Karbala? Haujafika wakati wa kuondoa bendera nyekundu kwenye kaburi la babu yako Hussein? Lini tutasikia wito ukisema (Enyi walipizaji wa kisasi cha Hussein)?
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: