Hospitali ya Alkafeel imeonyesha utayari wa kutibu waandamanaji na askari wanaojeruhiwa kwenye maandamano.

Maoni katika picha
Idara ya hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza utayari wa kutibu bure waandamanaji na askari wanao jeruhiwa kwenye maandamano, imekua ikifanya hivyo tangu siku ya kwanza ya maandamano, milango yake imeendelea kuwa wazi muda wote, haijawahi kukataa mgonjwa yeyote.

Hayo yapo katika barua iliyotumwa na uongozi wa hospitali hiyo katika ofisi za afya za mkoa wa Karbala, ifuatayo ni sehemu ya nakala ya barua hiyo:

(Kutokana na hali ya mji wa Karbala kwa sasa, na matukio yanayo endelea kushuhudiwa, tunapenda kuwajulisha kua hospitali ipo tayali kutoa huduma za matibabu bure kwa watu wanao jeruhiwa kwenye maandamano, sawa wawe ni waandamanaji au askari).

Imebainisha kua wagonjwa wanao pokelewa hupelekwa hospitali ya Safiir au Imamu Hussein (a.s) na huo ndio mkakati wa afya uliopangwa na wizara ya afya ya Iraq.

Kumbuka kua hospitali ya Alkafeel ilikua imeha toa tamko kwanba milango yake ipo wazi kwa ajili ya kutibu wairaq wote, imesha tibu watu wengi walio jeruhiwa kwenye maandamano, kuanzia waandamanaji hadi askari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: