Kamati ya maandalizi: Kuahirishwa kwa kongamano la makumbusho ya Alkafeel ya kimataifa awamu ya tatu hadi itakapo tangazwa tena.

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la makumbusho ya Alkafeel ya kimataifa awamu ya tatu, lililokua limepangwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi ujao limeahirishwa hadi itakapo tangazwa tena, kutokana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa.

Kumbuka kua kamati ilitangana kukamilika kwa maandalizi yote ya kongamano hilo chini ya kauli mbiu isemayo (Makumbusho na fani za kisasa) kukiwa na mada zifuatazo:

  • - Njia za kuhifadhi elimu ya makumbusho.
  • - Makumbusho katika mitandao ya mawasiliano ya kijamii.
  • - Njia za kisasa katika maonyesho ya makumbusho.
  • - Elimu na njia za kisasa katika kulinda majengo ya makumbusho.
  • - Njia na vifaa vya kisasa katika kupangilia makumbusho.
  • - Kuboresha kazi ya usimamizi wa makumbusho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: