Kuondoa mandhari ya huzuni iliyo dumu miezi miwili Muharam na Safar katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maoni katika picha
Kama kawaida katika kupokea mwezi wa Rabiul-Awwal na kuaga msimu wa huzuni ambao hudumu miezi miwili Muharam na Safar, watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanaondoa mapambo meusi.

Kazi hiyo ilianza kwa kubadilisha bendera kwenye kubba takatifu, kwa kuondoa nyeusi na kuweka nyekundu, sambamba na kuondoa alama zote zinazo ashiria huzuni ikiwa ni pamoja na vitambaa vyote vyeusi vikubwa na vidogo, aidha haram imesafishwa na kutandikwa mazuria mapya na kupuliziwa marashi.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu huwekwa mapambo meusi katika kipindi cha miezi miwili kila mwaka, ambayo ni mwezi wa Muharam na Safar, kama alama ya kuomboleza msiba wa watu wa nyumba ya Mtume Muhammad walio pata katika miezi hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: