Miswala mipya yatandikwa ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maoni katika picha
Baada ya kumaliza msimu wa huzuni za Husseiniyya uliodumu kwa kipindi cha miezi miwili Muharam na Safar, kama kawaida ya Atabatu Abbasiyya tukufu, watumishi wa kitengo cha kusimamia haram tukufu wanafanya kazi ya kutandika miswala mipya ndani ya ukumbi wa haram tukufu, kama ishara ya kuingia kwa mwezi wa Rabiul-Awwal, kazi hiyo inafanywa sambamba na kusafishwa pamoja na kupuliza marashi.

Kuhusu kazi hiyo tumeongea na makamo rais wa kitengo cha kusimamia haram tukufu bwana Haadi Mahadi Muhammad amesema kua: “Saa za mwisho za mwezi wa Safar tulianza kazi ya kutandika miswala mipya ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), tumetandika zaidi ya miswala elfu moja katika eneo lenye ukubwa wa (2m6000), kabla ya kutandika miswala hiyo tulianza kupiga deki pamoja na kupuliza marashi”.

Akaongeza kua: “Miswala iliyo tandikwa –kama inavyo julikana- ni ya kifahari yenye ubora mkubwa, ina rangi nzuri iliyotiwa nakshi za kiislamu zinazo endana na utukufu wa eneo hili”.

Kumbuka kua kitengo cha kusimamia haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya ni jukumu lake kupiga deki na kutandika miswala ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kazi hiyo ipo katika ratiba maalum ya majukumu yake, hasa baada ya ziara ya Arubaini kila mwaka kutokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Ataba tukufu, hutandika miswala bora zaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: