Ni desturi ya chama cha washairi na waimbaji wa Husseiniyya katika mkoa wa Karbala, kufanya maukibu (matembezi) ya kuomboleza katika siku ya mwisho ya mwezi wa Safar, ambayo huanzia barabara ya Kibla ya Imamu Hussein (a.s) hadi katika haram tukufu ya baba wa watu huru -Abul-Ahraar- (a.s), kisha huelekea katika malalo ya mbeba bendera ya Twafu mwezi wa bani Hashim (a.s) wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, na kuhitimisha matembezi hayo ndani ya haram yake kwa kufanya majlisi ya kuomboleza.
Yamekua mazowea kwa watumishi wa mimbari ya Imamu Hussein (a.s) kwa sababu wao siku zote ndani ya miezi miwili Muharam na Safar hushughulika na mimbari, hawapati nafasi ya kutoka rasmi na maukibu ya kuwapa pole watu wa nyumba ya Mtume (a.s) katika msiba huu.
Kumbuka kua chama hiki kilianzishwa na marehemu wawili waliokua watumishi wa Hussein (a.s), mshairi mkubwa Shekh Kaadhim Almandhuur na muimbaji maarufu Hamza Zaghiir katika miaka ya sabini karne iliyo pita, baada ya kuzuwiliwa na kushambuliwa harakati zote za watumishi wa Imamu Hussein (a.s) na utawala wa kidikteta uliopita, harakati nyingi zilisimama, baada ya kuanguka utawala huo na kwa utukufu wa mtumishi mzalendo wa Imamu Hussein (a.s) katika mji wa Karbala ambaye alikua baba wa kiroho marehemu muimbaji na mshairi Muhammad Hamza (r.a) zilirudishwa upya harakati za chama hiki.