Idara ya kupotelewa chini ya kitengo cha zawadi na nadhiri cha Atabatu Abbasiyya tukufu, imetoa wito kwa mazuwaru wote walio tembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wakati wa ziara ya Arubaini na wakapoteza vitu vyoa, wawasiliane na ofisi ya idara hiyo iliyopo ndani ya Ataba tukufu kwa simu namba (009647804947331) au kwa kutumia barua pepe: lost@alkfeel.net aidha idara imesema kua zaairu anaweza kuangalia vitu vilivyo okotwa kupitia linki hii: https://alkafeel.net/lost/.
Kumbuka kua mtandao wa kimataifa Alkafeel unaukurasa maalum wa waliopotelewa (alkafeel.net/lost) ukurasa huo unatoa fursa kwa mtu yeyote aliye poteza kitu chake ndani ya Atabatu Abbasiyya au maeneo ya jirani na Ataba ya kurahisishiwa kurudishiwa mali yake, sawa iwe ni kito cha thamani, pesa, beji, simu, kamera au kitu chochote kile kama vile (vitambulisho, hati ya kusafiria na vinginevyo).