Muhimu na imetokea hivi sasa.. Nakala ya tamko la Marjaa Dini mkuu kuhusu hali ya Iraq kwa sasa.

Maoni katika picha
Muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu kwenye khutuba ya swala ya Ijumaa leo (3 Rabiul-Awwal 1441h) sawa na (1 Novemba 2019m) iliyo swaliwa ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), amesoma nakala iliyo tolewa na ofisi ya Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu.

Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amesema kua:

Mabwana na mabibi nakusomeeni nakala iliyo tufikia kutoka ofisi ya Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani katika mji wa Najafu.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.

Pamoja na kuendelea maandamano ya wananchi wanaodai islahi katika mji wa Bagdad na miji mingine, wiki hii tumeshuhudia matukio mapya ya kuumiza na kusikitisha kati ya waandamanaji na wanamshikamano na kati ya askari na watu wengine, umetokea umwagaji wa damu na kujeruhiwa idadi kubwa pande zote, sambamba na matukio ya uchomaji moto na uporaji wa mali za umma na binafsi.

Hakika damu zilizo mwagika wiki za nyuma ni tukufu kwetu wote, lazima tufanye kila tuwezalo kuzuwia umwagaji wa damu, tusiruhusu kuliingiza taifa katika mauwaji ya sisi kwa sisi, virugu na uharibufu, itawezekana kuzuwia janga hili iwapo tukishirikiana kwa dhati na kutanguliza mapenzi ya taifa la Iraq na mustakbali wake.

Hakika Marjaa Dini mkuu anasisitiza tena msimamo wake maarufu wa kulaani kushambuliwa kwa watu wanaofanya maandamano ya amani, na umuhimu wa kuchukuliwa hatua watu wanaofanya hivyo, anawaomba wenye mamlaka kuacha kuwatuma wanajeshi kwenda kupambana na watu wanao andamana kwa amani, ili kuepusha maafa zaidi. Inatakiwa kuheshimu matashi ya wairaq kuhusu uchaguzi wa mlengo wa siasa na utawala wanao taka katika taifa lao, kwa kupiga kura ya maoni kuhusu katiba na uchaguzi wa bunge, huo ndio msimamo wa Marjaa Dini mkuu, amekua akisisitiza jambo hilo tangu ulipo angushwa utawala uliopita, leo anasisitiza kua islahi ni jambo la lazima –kama ilivyo zungumzwa zaidi ya mara moja- jambo muhimu katika islahi pia ni kuwapa uhuru raia wote wa Iraq bila kuangalia tabaka zao na milengo yao, wa kuchagua mlengo wa siasa na aina ya utawala wanaotaka, haitakiwi kwa mtu yeyote au kikundi chochote au mlengo fulani, kitongoji fulani au taifa fulani kuwapangia wairaq na kulalimisha maoni yake.

Tunawaomba wananchi wote mtafakari hali ya Iraq kwa sasa na baadae, wala msirubuniwe na yeyote na kuacha kufanya maamuzi sahihi kuhusu jambo hili, angalieni maslahi ya taifa na mustakbali wake, Mwenyezi Mungu atawaongoa katika haki naye ni mkuu wa kuwafikisha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: