Katika kuendelea kusaidia watu wanao andamana kwa amani kudai haki zao: Atabatu Abbasiyya tukufu yafungua kituo cha afya katika uwanja wa waandamanaji mjini Karbala

Maoni katika picha
Katika kuunga mkono watu wanaofanya maandamano ya amani kwa ajili ya kudai haki zao walizo pewa na katiba ya Iraq na kupasishwa na Marjaa Dini mkuu, Atabatu Abbasiyya tukufu imefungua kituo cha afya katika uwanja wa watu wanaofanya maandamano ya amani katika mkoa wa Karbala, ili kutoa matibabu kwa majeruhi wa maandamano raia au askari.

Jambo hili ni muendelezo wa huduma zingine zinazo tolewa na Ataba, kama vile kugawa chakula, maji safi ya kufanywa, sambamba na huduma za matibabu zinazo tolewa na hospitali ya rufaa Alkafeel ambayo inapokea watu waliojeruhiwa kwenye maandamano, imefanikiwa kutibu maelfu ya wahanga wa maandamano huku wengine ikiwapeleka hospitali ya Husseini au Safiir, bado inaendelea na kazi hiyo hadi sasa.

Kituo kinaendeshwa na madaktari bingwa na wauguzi mahiri kutoka hospitali ya rufaa Alkafeel, wakiwa na vifaa vyote vya lazima katika kazi hiyo, kituo hicho kinafanya kazi muda wote, aidha wame egesha gari za wagonjwa pembezoni mwa waandamanaji.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa huduma mbalimbali kwa waandamanaji, kama vile:

  • - Kugawa chakula kutoka kwenye mgahawa wa Atabatu Abbasiyya ambacho hupelekwa kwa waandamanaji kwa kutumia gari maalum.
  • - Kugawa maji ya kunywa.
  • - Kugawa juisi, matunda na chai kwa mida tofauti wakati wa mchana.
  • - Kutuma gari maalum za kufanya usafi kwenye maeneo yanayo tumiwa na waandamanaji.
  • - Kufungua vituo vya kugawa maji safi kwa waandamanaji.
  • - Kutibu watu wanaopata matatizo ya afya katika maandamano waandamanaji au askari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: