Jiko la jengo la Alqamiy linaandaa chakula na kukigawa kwa waandamanaji wa Karbala

Maoni katika picha
Katika kufuata nyayo za Atabatu Abbasiyya tukufu ambayo inaandaa chakula na kukigawa kwa waandamanaji wa Karbala wanao dai haki zao za kisheria walizo pewa na katiba ya Iraq na kuungwa mkono na Marjaa Dini mkuu, kutokana na wingi wa chakula wanacho andaa ukizingatia kua wanatakiwa kugawa chakula kwa Mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s), ndipo jiko la jengo hilo likapewa jukumu la kuandaa chakula chini ya ratiba iliyo andaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, sawa kiwe chakula cha mchana au usiku, sambamba na kugawa matunda na juisi pamoja na maji ya kunywa, chakula hupelekwa na gari maalum kwa waandamaji, kila mtu hupewa chakula kikiwa kwenye kifungashio, vifungashio hivyo hurahisisha ugawaji wa chakula, watumishi wa jengo hilo pamoja na wale wa Atabatu Abbasiyya tukufu ndio husimamia ugawaji wa chakula hicho.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa huduma mbalimbali kwa waandamaji, miongoni mwa huduma hizo ni:

  • - Kuandaa maelfu ya sahani za chakula katika mgahawa wa Ataba na kwenda kukigawa kwa waandamanaji kwa kutumia gari maalum.
  • - Wanagawa maelfu ya chupa za maji ya kunywa.
  • - Wanagawa matunda, juisi na chai kwa nyakati tofauti.
  • - Wanafanya usafi kwa kutumia gari maalum za usafi katika maeneo yanayo tumiwa na waandamanaji.
  • - Wamefungua vituo vya kugawa maji safi na salama kwa waandamaji.
  • - Wamefungua vituo vya kutoa huduma za matibabu kwa waandamanaji na askari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: