Kutokana na kuendelea kwao kuunga mkono watu wanaofanya maandamano ya amani na kudai haki zao walizo pewa na katiba na kuungwa mkono na Marjaa Dini mkuu, jioni ya Jumamosi (4 Rabiul-Awwal 1441h) sawa na (2 Novemba 2019m), watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wametoka na kuungana na watu wanaofanya maandamano ya amani yanayo shuhudiwa katika mikoa tofauti ya Iraq pamoja na Karbala.
Maandamano yalianzia katika mlango wa Kibla wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), idadi kubwa ya watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wakiongozwa na katibu wao mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar pamoja na naibu wake na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi bila kuwasahau maraisi wa vitengo, wameshiriki kwenye maandamano hayo, wamekatisha katika mji mkongwe na kuelekea sehemu ambayo waandamanaji wameweka kambi katikati ya mji wa Karbala, huku wakiwa wamebeba bendera za Iraq na mabango mbalimbali ya kudai haki, na kuimba mimbo ya kuonyesha kulipenda taifa lao, maandamano hayo yakaishia katika jengo la serikali ya mkoa wa Karbala, sehemu ambayo wamewasilisha madai yao ya kutaka kutekelezwa matakwa ya wananchi wa Iraq.
Fahamu kua Atabatu Abbasiyya tukufu kwa siku kadhaa, imekua ikitoa misaada mbalimbli kwa waandamanaji wa mkoa wa Karbala, kama vile chakula, maji ya kunywa na mingineyo, viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanakubali haki ya kufanya maandamano ya amani kwani ipo kikatiba na imeungwa mkono na Marjaa Dini mkuu.