Maahadi ya Quráni tukufu / tawi la Hindiyya imefanya kikao cha usomaji wa Quráni tukufu kwa ajili ya kumkumbuka msomaji mkubwa wa mahadhi ya kiiraq, ambaye ni marehemu Ustadh Abbasi Juma, kwa kushirikiana na kikosi cha mwangi wa haki.
Kiongozi wa tawi la Maahadi Sayyid Haamid Marábiy ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kikao cha usomaji wa Quráni ni sehemu ya harakati za tawi hili, tumefanya kisomo hiki kama sehemu ya kumkumbuka mtu aliyekua msomaji mkubwa wa Quráni katika wilaya hii, kikao kilifunguliwa kwa Quráni iliyo somwa na Haafidh Karim Al-Handawi, kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya marehemu na mashahidi wa Iraq, halafu ukafuata ukaribisho ulio tolewa na Ustadh Abdul-Haadi Zaár na akasoma wasifu wa marehemu, ambapo alieleza historia yake kimalezi na kielimu.
Akaongeza kua: “Hafla ilipambwa na wasomaji wa mahadhi ya kiiraq, ambao ni Yusufu Fatalawi na Hassan Janabi, pia yakatolewa maelezo kuhusu usomaji wa mahadhi ya kiiraq, na kwa mara ya kwanza alialikwa mchoraji mahiri ambaye alichora picha ya marehemu”.