Kumaliza kazi ya kusafisha paa la vioo katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maoni katika picha
Kitengo cha usimamizi wa haram katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimemaliza kazi ya kuosha paa la vioo katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na kuosha sehemu zingine za vioo, kazi imekamilishwa ndani ya muda uliopangwa, kiliteuliwa kikosi maalum kwa ajili ya kazi hiyo, kazi zilizo fanywa ni:

  • - Kusafisha miinuko yote ya paa la vioo kwa kutumia maji maalum yanayo fanya lionekane safi muda wote.
  • - Kutengeneza baadhi ya sehemu zilizo haribika kwenye paa.
  • - Kukagua na kurekebisha sehemu za umeme.
  • - Kusafisha sehemu zote za vioo pamoja na zile zinazo tenganisha sehemu moja na nyingine.
  • - Kusafisha vumbi kwenye kubba zote zilizopo juu ya paa.

Fahamu kua paa ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) inamiinuko ya vioo (37) imefungwa bomba maalum za maji ambazo hutumika kusafishia, kuna mitambo minne iliyo wekwa katika nguzo za paa, ambayo hutumika kusukuma maji juu ya paa kila moja inauwezo wa (75) na husukuma maji kwa nguvu kupitia bomba zilizopo juu ya paa, maji hayo husambazwa kwenye miinuko ya vioo kisha kuna njia maalum ya kutoa nje maji hayo, njia hiyo hiyo ndio hutumika kutoa maji ya mvua pia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: