Hospitali ya Alkafeel inaendelea kuwatibu waandamanaji bure na yasisitiza kua: imesha tibu makumi ya watu wakiwemo waliokua na matatizo makubwa na hatari.

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kutoa matibabu kwa watu wanaofanya maandamano ya amani kudai haki zao walizopewa na katiba na kuungwa mkono na Marjaa Dini mkuu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyo tolewa na idara ya hospitali ya Alkafeel kwenye mtandao wa Alkfeel: “Tangu siku za kwanza za maandamano haya katika mji wa Karbala, hospitali ya rufaa Alkafeel ilifungua milango yake na kuanza kutoa matibabu kwa kila muandamanaji aliyefika hospitalini hapo kwa ajili ya kuhitaji matibabu kama ilivyo elekezwa na wizara ya afya ya Iraq, sanjari na hospitali ya Safiir na Husseini”.

Akabainisha kua: “Wamepokelewa makumi ya wagonjwa kutoka kwa waandamanaji miongoni mwao wakiwa katika hali mbaya zaidi na wote wametibiwa bure”.

Akafafanua kua: “Pamoja na tuliyo sema, hospitali inashiriki katika mkakati wa Atabatu Abbsiyya tukufu wa kutoa huduma kwa waandamanaji, kupitia vituo vya afya vilivyo funguliwa kwenye sehemu ambazo waandamanaji wameweka kambi, hivyo kila siku wanatibu makumi ya wagonjwa miongoni mwa waandamanaji na askari”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa misaada mbalimbali kwa waandamanaji, miongoni mwa misaada hiyo ni:

  • - Kuandaa maelfu ya sahani za chakula katika mgahawa wa Ataba na kwenda kukigawa kwa waandamanaji kwa kutumia gari maalum.
  • - Wanagawa maelfu ya chupa za maji ya kunywa.
  • - Wanagawa matunda, juisi na chai kwa nyakati tofauti.
  • - Wanafanya usafi kwa kutumia gari maalum za usafi katika maeneo yanayo tumiwa na waandamanaji.
  • - Wamefungua vituo vya kugawa maji safi na salama kwa waandamaji.
  • - Wamefungua vituo vya kutoa huduma za matibabu kwa waandamanaji na askari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: