Sauti ya raia: Haya ndio aliyosema Marjaa Dini mkuu tarehe (13 mei 2011m).

Maoni katika picha
Sauti ya raia wa kwanza iliyo pinga ufisadi uliojaa katika taasisi za serikali, mtu wa kwanza aliyepinga uzembe uliopo katika vyombo vya serikali, na mtu wa kwanza aliyetahadharisha kupuuzwa kwa madai ya raia ni Marjaa Dini mkuu, hili lipo wazi kwa kila anayefuatilia khutuba zake za miaka ya nyuma.

Tunataja mambo muhimu yaliyo semwa na Marjaa katika khutuba ya Ijumaa (9 Jamadal-Aakhar 1432h) sawa na (13 Mei 2011m), iliyo tolewa na Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai katika ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s), alivitaka vyama vyote vya siasa kuacha kudharau madai ya raia.

Na akaongea kuhusu swala la kupunguza mishahara ya wabunge, mawaziri na viongozi wakuu serikalini, akasema kua mishahara na posho za viongozi wakuu serikalini ni sehemu ya ubadhirifu wa mali za serikali, aidha alisema kua hakuna umuhimu wa kuongeza idadi ya wabunge, akasisitiza kua swala la kupunguza mishahara ya wabunge lifanywe kwa dhadi na wala sio juujuu kama ilivyo fanyika.

-Wakati ule- Marjaa Dini mkuu alitahadharisha vyama vyote vya siasa viache kupuuza madai ya wananchi, akasema kua jambo hilo ni hatari kwa mustakbali wa vyama vyote vya siasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: