Atabatu Abbsiyya tukufu yaomboleza mmoja wa watumishi wake aliye uwawa kwa kupigwa risasi na askari asiye muaminifu.

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu leo siku ya Jumatatu (6 Rabiul-Awwal 1441h) sawa na (4 Novemba 2019m) unatangaza msiba kwa kufiwa na mmoja wa wafanyakazi wake aliye pigwa risasi na askari asiyekua muaminifu, lifuatalo ni tamko la taarifa ya msiba huo:

Kwa majonzi na masikitiko makubwa, Atabatu Abbasiyya tukufu inatangaza msiba kwa kufiwa na mtumishi wake Ali Hussein Ahmadi Tamimi, aliyepigwa risasi na askari asiyekua muaminifu akiwa barabarani wakati anampelekea dawa mama yake.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu amrehemu yeye na mashahidi wote, tunaomba vyombo vya ulinzi na usalama vifichue njama ya kuuwawa kwake pamoja na kuuwawa kwa baadhi ya watu wanaofanya maandamano ya amani, katika maeneo tofauti ya Iraq.

Mwenyezi Mungu ainusuru Iraq na raia wake dhidi ya maadui zao.

Hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: