Kumbukumbu iumizayo: Mwezi nane Rabiul-Awwal alikufa kishahidi Imamu Hassan Askariy (a.s).

Maoni katika picha
Mwezi nne Rabiul-Awwal ni siku aliyo uwawa kishahidi Imamu wa kumi na moja Abuu Muhammad Hassan bun Ali bun Muhammad bun Ali bun Mussa bun Jafari bun Muhammad bun Ali bun Hussein bun Ali bun Abuu Twalib (a.s), na jina lake la lakabu ni Askariy, Siraaji, Khaalisu, Swaamit, Taqiyyu, Zakiyyu, Naqiyyu… lakabu mashuhuri zaidi ni (Askariy), aliuwawa kwa sumu mwaka wa (260h).

Alichukua rasmi madaraka ya Uimamu baada ya kifo cha baba yake Imamu Ali Haadi (a.s) mwaka wa (253h), utawala wa Abbasiyya haukumpa nafasi Imamu Hassan Askariy (a.s), walimuweka chini ya usimamizi mkali wakati wote, walidhibiti harakati zake zote, ili kumzuwia kutekeleza wajibu wake wa kuongoza umma, Imamu alitumia njia ya siri katika kufikisha ujumbe pamoja na kutumia mawakala, ushahidi wa kihistoria unaeleza kwa undani njia aliyo tumia Imamu (a.s).

Imamu Hassan Askariy (a.s) alikua sawa na baba zake (a.s) alipiga vita dhulma na ugaidi, akapambana kulinda misingi sahihi ya uislamu, jambo hilo liliwagharimu sana, walifungwa wakateswa na kuwekwa chini ya ulinzi.

Aliishi katika zama za watawala watatu wa bani Abbasi: Mu’taz, Muhtada na Ma’tamad, wote walimuweka chini ya ulinzi mkali na kumnyanyasa, mtawala wa mwisho alikua ni Mu’tamad, alikua muovu mpenzi wa mziki na mambo ya haram, watu wengi walikua hawampendi, Imamu akafanyiwa maudhi mengi na Mu’tamad, alimtenga na watu na akazuwia asionane na mtu yeyote, alikua anaogopa kuzaliwa kwa Imamu Mahadi msubiriwa, ambaye walikua wanajua kua atazaliwa na Imamu Hassan Askariy (a.s).

Na mwisho akaamua kumuua Imamu (a.s) kwa sumu kali iliyo muuguza kwa siku kadhaa hadi akafariki akiwa na miaka ishirini na nane, kifo chake kilitokea mwaka wa (260h).

Alizikwa pamoja na baba yake Imamu Haadi (a.s) kwenye nyumba yake katika mji wa Samaraa, malalo yao hutembelewa na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kutoka kila sehemu ya dunia, na hutabaruku na kutawasal kwa Mwenyezi Mungu kupitia utukufu wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: