Katika kuomboleza kifo cha Imamu Askariy (a.s): Mawakibu za kuomboleza za Karbala zinamiminika kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maoni katika picha
Asubuhi ya jana (8 Rabiul-Awwal 1441h) sawa na (6 Novemba 2019m) mawakibu za watu wa Karbala zimemiminika katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s) na kumpa pole kwa msiba huu yeye pamoja na Imamu Hujjat bun Hassan Mahadi (a.f).

Mawakibu zilianzia matembezi yao katika mji mkongwe zikaelekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kumpa pole wakiwa ndani ya haram yake tukufu halafu zinakwenda katika malalo ya bwana wa mashahidi (a.s), wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu huku wakiimba kaswida za kuomboleza msiba huu, na matembezi yao kuishia ndani ya haram ya bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein (a.s).

Fahamu kua mawakibu za kuomboleza za Karbala zinakawaida ya kufanya matembezi katika kila tukio la msiba unaohusu watu wa nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kutoa pole kwa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na kuhuisha utiifu kwao na kwa Imamu Mahadi msubiriwa (a.f).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: