Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Askariy (a.s).

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya jana Jumatano (8 Rabiul-Awwal 1441h) sawa na (6 Novemba 2019m) imefanya majlisi maalum kwa wafanyakazi wake ya kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s), ndani ya ukumbi wa utawala, ni kawaida yake kufanya hivyo katika kila tukio la kufiwa na Imamu mtakasifu (a.s).

Majlisi ilifunguliwa kwa Quráni tukufu, kisha Sayyid Adnani Mussawi kutoka kitengo cha Dini akatoa mawaidha, akaeleza mambo muhimu katika uhai wa Imamu Askariy (a.s), na kazi kubwa aliyo fanya ya kupambana na fikra potofu zilizo kua zinalenga kuharibu mafunzo ya uislamu halisi kwa wakati huo, sambamba na uadui alio fanyiwa Imamu (a.s) na namna alivyo wekwa chini ya ulinzi mkali kwa ajili ya kunyamazisha sauti ya haki, kisha akaeleza kisa cha kuuwawa kwake chini ya mfalme muovu.

Majlisi ikahitimishwa kwa kusoma kaswida na tenzi za kuomboleza msiba huu unaoumiza roho za watu wa nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na waumini wote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: