Nyoyo zilizojaa machungu na huzuni, adhuhuri ya jana Jumatano (8 Rabiul-Awwal 1441h) sawa na (6 Novemba 2019m) watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wamefanya matembezi ya kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s), matembezi yalianzia ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), watumishi wa mwezi wa bani Hashim (a.s) walisimama kwa mistari na kuimba kaswida za kuomboleza msiba huu unaoumiza watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w).
Baada ya hapo wakaanza kutembea wakielekea katika malalo ya bwana wa mashahidi (a.s) wakipita katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu huku wakipiga matam na kutokwa machozi, wakiwa na huzuni kubwa, walipo wasili katika haram ya Imamu Hussein (a.s) wakapokelewa na watumishi wa haram hiyo, halafu wakafanya majlisi ya pamoja ndani ya haram ya Abu Abdillahi Hussein (a.s) na mazuwaru waliokua sehemu hiyo wakashiriki kwenye majlisi hiyo.
Kumbuka kua Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya hufanya matembezi ya kuomboleza katika kila tukio la kufariki mtu miongoni mwa Ahlulbait (a.s) kipindi chote cha mwaka.