Katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s): Mazuwaru wa kike wanamuomba Mwenyezi Mungu alipe amani taifa la Iraq.

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya wa kike katika Atabatu Abbasiyya inafanya kumbukumbu ya kuvishwa taji Imamu Mahadi msubiriwa (a.f), wamefanya hafla ya kuadhimisha tukio hilo na kumuomba Mwenyezi Mungu kwa utukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s) alijalie taifa la Iraq na raia wake amani na utulivu, hayo yamefanywa ndani ya sardabu ya Imamu Jawaad (a.s) katika haram takatifu ya Abbasi.

Mtandao wa kimataifa Alkafeel umeongea na makamo kiongozi wa idara hiyo, bibi Taghridi Abdulkhaliq Atwiyya Tamimi amesema kua: Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya inakawaida ya kuadhimisha matukio ya kuzaliwa kwa maimamu watakasifu (a.s) na matukio mengine, likiwemo hili la kuvishwa taji kwa Imamu Mahadi (a.s) ambalo mwaka huu limesadifu wakati ambao Iraq inapita katika mazingira mgumu, jambo ambalo limetusukuma kumuomba Mwenyezi Mungu kwa utumufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na baraka za Imamu Mahadi (a.f) alijalie taifa la Iraq na raia wake amani na utulivu, na awarehemu mashahidi na kuwaponya haraka majeruhi.

Akabainisha kua: “Wameshiriki mazuwaru wengi kwenye program hii, kulikua na muhadhara kuhusu hali ya taifa kwa sasa, halafu ikasomwa Duaul-Ahadi na Duaul-Faraji kwa pamoja”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: