Wanaunga mkono madai ya watu wanaofanya maandamano ya amani: Watumishi wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) wanafanya maandamano ya pamoja.

Maoni katika picha
Alasiri ya Alkhamisi (9 Rabiul-Awwal 1441h) sawa na (7 Novemba 2019m) watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya walifanya maandamano ya pamoja kuunga mkono watu wanaofanya maandamano ya amani na kudai haki zao, idadi kubwa ya watumishi wa Ataba mbili paloja na viongozi wao wamefanya maandamano huku wakibeba bendera za Iraq na mabango yaliyo andikwa madai ya wananchi wa Iraq.

Maandamano yalianzia katika mlano wa Kibla kwenye haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuelekea upande wa mlango wa Kibla wa haram ya Imamu Hussein (a.s), hapo wakakutana watumishi wa Ataba zote mbili tukufu, halafu wakaelekea katika uwanja wa maandamano ndani ya mji mtukufu wa Karbala, kuungana na waandamanaji wengine pamoja na kuunga mkono madai yao ya kisheria.

Fahamu kua Ataba zote mbili wiki iliyo pita zilifanya maandamano pia, kuonyesha kuunga kwao mkono maandamano ya amani yanayo fanyika Karbala na kwenye mikoa mingine ya Iraq, bila kusahau Ataba zote mbili zinatoa huduma mbalimbali kwa waandamanaji, ikiwa ni pamoja na kugawa chakula na vinywaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: