Kikosi cha shambaboy cha Alkafeel chaanza kazi ya kuchambulia miti iliyopo kwenye barabara za mji mtukufu wa Karbala.

Maoni katika picha
Mradi wa miti ya barabarani na maeneo ya katikati ya mji wa Karbala ni moja ya miradi inayo tekelezwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, bado inaendelea nao kwa lengo la kupanda miti kwenye barabara zote na maeneo ya wazi, kazi hiyo inafanywa na jopo la shambaboy wa Alkafeel, na haiishii kwenye kupanda miti peke yake, bali kuna kazi zingine kama vile kumwagilia, kubadilisha miti iliyo fubaa au kuharibika, sambamba na kuendelea kuiweka katika mazingira mazuri, ikiwa ni pamoja na kuichambulia.

Jopo la shambaboy wa Alkafeel limeanza kazi ya kuchambulia miti iliyopo pembezoni mwa barabara za mkoa mtukufu wa Karbala pamoja na maeneo ya wazi yaliyo pandwa miti siku za nyuma, katika mradi wa upandaji miti unaofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kazi haijaanza muda mrefu, pia inafuatia uharibifu wa miti hiyo uliotokea ndani ya kipindi cha ziara ya miezi miwili: Muharam na Safar, kwa ajili ya kupendezesha muonekano wake, kikosi cha shambaboy cha Alkafeel kimeanza kufanya kazi hii inayo husisha:

  • - Kuchambulia miti kwa mitindo mizuri inayo endana na kipindi hiki.
  • - Kuondoa miti iliyo haribika na kupanda miti mingine.
  • - Kuandaa upya sehemu za kupanda miti.
  • - Kusamadia sehemu za kupanda miti.
  • - Kukagua barabara zinazo hitaji kupandwa miti na kubaini sehemu za kuipanda.

Kumbuka kua kazi hii ni sehemu ya mradi wa shambaboy wa Atabatu Abbasiyya tukufu, wanajukumu la kupanda miti katika mji mtukufu wa Karbala, na kuhakikisha mji unakua na muonekano mzuri, unao endana na hadhi yake katika nyoyo za waislamu na walimwengu kwa ujumla, na kuufanya uvutie kwa mazuwaru na wakazi, miti yote mikubwa na midogo ya kivuli na ya mauwa iliyopo ndani ya mji huu inatokana na kazi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: